Announcements

Posted On: Aug 22, 2023


UPUNGUFU WA HUDUMA YA MAJI KWA WAKAZI WA WANAOHUDUMIWA NA MTAMBO WA RUVU JUU


21.08.2023

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) inawatangazia wateja na Wananchi wanaohudumiwa na mtambo wa kuzalisha maji Ruvu juu kuwa, kutakuwa na upungufu wa huduma ya maji kwa muda wa saa kati ya 12 na 24 kwa siku ya Jumatatu tarehe 21.08.2023 hadi Jumanne tarehe 22.08.2023.

Sababu: Kuruhusu matengenezo ya pampu za kusukuma maji mtamboni

Maeneo yatakayoathirika ni;
Ruvu darajani, Ruvu JKT, Mlandizi, Mbwawa, Visiga, Mile 35, Misugusugu, Kongowe, Soga, Miembe saba, Kwa Mfipa, Mwendapole, Tanita, Kwa Mathias, Kwa Mbonde, Picha ya ndege, Lulanzi, Kibaha, Kiluvya, Kibamba, Mbezi, Magari Saba, Mbezi inn, Mbezi, Kimara,Tabata, Kinyerezi, Kisukuru, Msigani, Maramba mawili, Tabata, Kimara B, Kimara Korogwe, Bucha, Baruti,Ubungo, Kisarawe, Ukonga, Pugu na Gongo la Mboto

Tafadhali kumbuka kuhifadhi maji ili kuweza kuyatumia katika kipindi cha matengenezo.

Tunaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.

Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kupitia kituo cha huduma kwa wateja 0800110064 (bure) au
0735 202 121(WhatsApp tu)

Imetolewa na
Kitengo cha Mawasiliano na Jamii

DAWASA