Wizara ya Maji

Dar es Salaam Water Supply And Sanitation Authority (DAWASA)

TIRA Logo
GOBA MPAKANI WABORESHEWA HUDUMA YA MAJI 
15 Sep, 2023
GOBA MPAKANI WABORESHEWA HUDUMA YA MAJI 

Zoezi la kulaza na bomba ya inchi 6, 4 na 3 ikitekelezwa kwa lengo la kusogeza huduma ya Majisafi kwa wakazi wa Goba mpakani ambao ni wanufaika wa mradi wa usambazaji maji Makongo hadi Bagamoyo

Kazi hii inayotekelezwa na mafundi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA)- Makongo inalenga kufikisha huduma kwa wakazi takribani 500 wa eneo hilo. 

Mradi wa maji Makongo hadi Bagamoyo ni miongoni mwa mradi wa kimkakati uliotekelezwa na Mamlaka kwa lengo la kutatua  changamoto ya upatikanaji wa maji hasa kwa wakazi wa Goba.