PAMPU MPYA ZAENDELEA KUFUNGWA RUVU JUU, KUIMARISHA HUDUMA
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar Es Salaam (DAWASA) imeendelea na zoezi la ufungaji wa Pampu mpya katika mtambo wa Uzalishaji maji Ruvu Juu, zenye lengo la kuimarisha uzalishaji na usambazaji wa maji katika Mkoa wa Dar Es Salaam na Pwani.
Akizungumza wakati akikagua endelevu za zoezi hilo, Mkurugenzi idara ya uzalishaji na usambazaji maji DAWASA, Mhandisi Ndele Mengo amemtaka Mkandarasi kuongeza kasi ili kuhakikisha pampu zote zinakamilika ndani ya muda uliopangwa na wananchi wanapata huduma ya maji.
"Katika mtambo huu tutafunga pampu nne (4) kati ya hizo pampu moja imekamilika na inafanya kazi tayari huku ufungaji wa pampu zilizobaki ukiwa katika asimilia 65, tunatarajia zoezi hili kukamilika ifikapo mwezi Septemba, 2026.
Mhandisi Mengo ameeleza kuwa kukamilika kwa zoezi hilo la ufungaji pampu, kutaongeza ufanisi katika uzalishaji wa maji na kupelekea uimarikaji wa huduma ya maji kwa wananchi wa Mikoa ya Dar na Pwani.
Katika hatua nyingine Mhandisi Mengo ameishukuru Serikali kwa uwekezaji unaofanyika katika mitambo ya uzalishaji maji kwani jitihada hizo zitakwenda kutatua changamoto za upatikanaji huduma ya maji kwa wananchi.
Ziara ya ukaguzi imefanyika katika Mtambo wa Uzalishaji Maji wa Ruvu Juu kukagua maendeleo ya ufungaji wa pampu mpya zinazolenga kuongeza na kuimarisha uzalishaji wa maji kwa wakazi wa Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani.
Kati ya pampu nne, pampu moja tayari imekamilika kufungwa na imeanza kufanya kazi, huku pampu nyingine tatu zikiwa katika hatua ya takribani asilimia 65 ya ufungaji.
Amesema kukamilika kwa mradi huo kutakuwa na mchango mkubwa katika kuongeza kiwango cha uzalishaji Maji na kuimarisha upatikanaji wa huduma ya majisafi kwa wananchi wa Dar es Salaam na Pwani.
Aidha, Mhandisi Mengo ameishukuru Serikali kwa uwekezaji unaofanyika katika Mtambo wa Uzalishaji Maji wa Ruvu Juu, akieleza kuwa hatua hiyo ni sehemu ya juhudi za kuendelea kuboresha miundombinu ya maji na kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora na ya uhakika
