Wizara ya Maji

Dar es Salaam Water Supply And Sanitation Authority (DAWASA)

TIRA Logo
USOMAJI NA UHAKIKI WA MITA ZA MAJI UNAENDELEA BAGAMOYO
14 Aug, 2024
USOMAJI NA UHAKIKI WA MITA ZA MAJI UNAENDELEA BAGAMOYO

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) kupitia Mkoa wa kihuduma Bagamoyo umeendelea kuwakumbusha wateja juu ya umuhimu wa usomaji na uhakiki mita pindi wanapo pokea wa usomaji kwenye simu zao ili kuongeza uwazi katika usimamizi wa utoaji huduma.

Akiongea na wakazi wa Kimarang'ombe kata ya Nianjema, Afisa Biashara wa DAWASA Bagamoyo, Ndugu Mwaka Miyeye amesema zoezi la usomaji mita kwa kushirikiana na wateja linaendelea sambamba na uhakiki wa usomaji ambapo wateja wanapata nafasi ya kuhakiki mita zao kabla ya kuandaliwa bili za mwezi.

"Zoezi la usomaji mita bado linaendelea na baadhi ya wateja tayari wameshapokea jumbe fupi za uhakiki wa usomaji, tunatoa rai kwa wateja wetu kuwa ni muhimu kuhakiki usomaji mita na kutoa taarifa kama kuna changamoto ili tuifikie kwa wakati. Taarifa hizo zinapokelewa kupitia mawasiliano namba za huduma kwa Wateja 0800110064 au wafike katika ofisi zetu ili kutatua changamoto." amesema Ndugu Miyeye.

Ndugu Miyeye amesisitiza ushirikiano kati ya wateja na Mamlaka ni muhimu hivyo anaendelea kuwasihi wateja kutoa ushirikiano kwa watumishi pindi wanapopita katika makazi yao.

Mkoa wa kihuduma DAWASA Bagamoyo una jumla ya wateja takribani 10,650 na unahudumia Kata za Yombo, Kisutu, Zinga, Nia njema, Dunda, Magomeni na Kiromo.