Wizara ya Maji

Dar es Salaam Water Supply And Sanitation Authority (DAWASA)

TIRA Logo
WAKAZI WA DUNDA WABORESHEWA HUDUMA YA MAJI
15 Feb, 2025
WAKAZI WA DUNDA WABORESHEWA HUDUMA YA MAJI

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) kupitia Mkoa wa Kihuduma wa Kisarawe inaendelea na kazi ya ubadilishaji wa miundombinu ya mabomba chakavu yaliyorithiwa kutoka katika Mradi wa Jamii wa GOPU kwa lengo la kuboresha upatikanaji wa huduma ya maji katika eneo la Dunda katika Kata ya Pugu.

Maboresho hayo yanahusisha ubadilishaji wa mabomba chakavu yenye kipenyo cha inchi 4", inchi 6" na inchi 8" kwa umbali wa kilomita mbili na yatasaidia kuondoa changamoto ya mivujo na ukosefu wa huduma ya maji kwa wakazi wa maeneo hayo.

Kukamilika kwa kazi hiyo kutaimarisha upatikanaji wa huduma ya maji kwa wakazi zaidi ya 1,200 waliopo katika maeneo ya Dunda A, Forest Hill, Pugu Bombani, Moravian na baadhi ya maeneo ya Bane.