Wizara ya Maji

Dar es Salaam Water Supply And Sanitation Authority (DAWASA)

TIRA Logo
ZOEZI LA MAUNGANISHO KWA WATEJA WAPYA LINAENDELEA MADALE - KULANGWA.
15 Feb, 2025
ZOEZI LA MAUNGANISHO KWA WATEJA WAPYA LINAENDELEA MADALE - KULANGWA.

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) kupitia Mkoa wa kihuduma DAWASA Mivumoni imeendesha zoezi la utoaji wa vifaa vya maunganisho mapya ya majisafi kwa wateja wa maeneo ya Goba, Tegeta A, Mivumoni, Madale, Nyakasangwe, Kisanga, Kilimahewa, Kinzudi, Kilimahewa juu, na Muungano ili wanufaike na jitihada za Serikali za kuhakikisha wanapata maji.

Mbali na zoezi la utoaji wa vifaa hivyo, DAWASA Kibamba imetoa elimu mbalimbali ikiwa ni pamoja na elimu ya utunzaji miundombinu ya maji, matumizi sahihi ya maji, njia rasmi za kimawasiliano, malipo ya ankara na huduma nyingine zitolewazo na Mamlaka.

Zaidi ya wateja wapya 100 wa maeneo hayo wanaenda kunufaika na huduma ya majisafi baada ya kukamilika kwa zoezi la maunganisho.

Kwa msaada zaidi wasiliana nasi kupitia kituo cha huduma kwa wateja 0800110064 (Bure) au 0735 355 755 DAWASA Mivumoni.