TAARIFA KWA UMMA - MATENGENEZO YA BOMBA CHANGANYIKENI NA MAKONGO
TAARIFA KWA UMMA
MATENGENEZO YA BOMBA CHANGANYIKENI NA MAKONGO
21.7.2026
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) inawatangazia Wateja na Wananchi wa maeneo ya Changanyikeni na Makongo, kutakuwa na ukosefu wa huduma ya Maji kwa muda wa Saa 9 kuanzia Saa 5 Asubuhi siku ya Jumanne, Julai 21, 2026 hadi Saa 2 Usiku.
Sababu: Kuruhusu matengenezo ya bomba la inchi 16 linalopeleka maji Changanyikeni kutoka Kituo cha Kusukuma maji Makongo.
Maeneo yatakayoathirika
Mtipesa, Kibululu, Ronda Mnalani, Kona Ajabu, Kingstone, Kwa Mongela, Shule ya Sekondari Makongo, Njia Panda Ronda, Kwa Njau, Barabara ya Mtaa wa Ng'ombe, Mtaa wa Atido, Downvialley , Kwa Diwani, Kwa Uombe na Serikali ya Mtaa Makongo Orlex, Mambosasa, Mbezi Madukani, St. Columbus, Chongoro, Kanisa Katoriki, Kwa Mlaki, Saiberia na George Washington
Tunaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.
Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kupitia kituo cha huduma kwa wateja
181 (bila malipo) au 0735 202 121(WhatsApp tu)
Imetolewa na
Kitengo cha Mawasiliano.
