Wizara ya Maji

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA)

TIRA Logo
TAARIFA KWA WAKAZI WA BUNJU NA MABWEPANDE - MATENGENEZO YA DHARURA YATAKAYOATHIRI UPATIKANAJI HUDUMA YA MAJI
28 Jul, 2026 Pakua

TAARIFA KWA WAKAZI WA BUNJU NA MABWEPANDE

MATENGENEZO YA DHARURA YATAKAYOATHIRI UPATIKANAJI HUDUMA YA MAJI

28.7.2026
 
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) inawataarifu Wananchi na Wateja wa Bunju na Mabwepande Wilaya ya Kinondoni kuwa kutakuwa na ukosefu wa huduma ya Maji kwa Saa 10 kwa siku ya Jumanne kuanzia Saa 4 Asubuhi hadi Saa 2 Usiku.

Sababu: Matengenezo ya dharura ya bomba lenye ukubwa wa inchi 16 katika eneo la tenki la Mabwepande.

Maeneo yatakayoathirika ni;
Bunju B, Bunju Mkoani, Kilungule, Mbopo, Mji mpya na Mpiji Magoe

DAWASA inaomba radhi kwa usumbufu utakaojitokeza wakati wa utekelezaji wa zoezi hili uliojitokeza.

Kwa maelezo zaidi, wasiliana nasi kupitia kituo cha huduma kwa wateja 181 (bila malipo) au 0735 202 121(WhatsApp tu) na 0734 315 600 (Huduma kwa Wateja, DAWASA Mabwepande)

Imetolewa na 
Kitengo cha Mawasiliano.