TAARIFA KWA WAKAZI WA MWENGE HADI KATIKATI YA MJI - MATENGENEZO YA DHARURA YATAKAYOATHIRI UPATIKANAJI HUDUMA YA MAJI
TAARIFA KWA WAKAZI WA MWENGE HADI KATIKATI YA MJI
MATENGENEZO YA DHARURA YATAKAYOATHIRI UPATIKANAJI HUDUMA YA MAJI
25.7.2026
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) inawataarifu Wananchi na Wateja wa maeneo ya Mwenge hadi katikati ya Maji, kuwa kutakuwa na ukosefu wa huduma ya majisafi kwa takribani saa 8.
Tarehe: Julai 25, 2026 kuanzia saa 3 Usiku hadi Julai 26, 2026 Saa 12 Asubuhi.
Sababu: Kuruhusu Matengenezo ya dharura ya bomba kubwa la inchi 12 eneo la Ubalozi wa Zambia.
Maeneo yatakayoathirika ni;
Oysterbay, Msasani, Masaki, Mikocheni, Makumbusho, Kijitonyama, Mwenge, Kinondoni, Mwananyamala, Magomeni, Moscow, Kariakoo, Posta, City Centre, Ilala na Hospitali ya Muhimbili.
DAWASA inaomba radhi kwa usumbufu utakaojitokeza.
Wasiliana nasi kupitia kituo cha huduma kwa wateja 181 (bila malipo) au 0735 202 121(WhatsApp tu)
Imetolewa na
Kitengo cha Mawasiliano.
