Wizara ya Maji

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA)

TIRA Logo
MRADI WA KUSAMBAZA MAJI KONGOWE HADI SOGA
MRADI WA KUSAMBAZA MAJI KONGOWE HADI SOGA

TAARIFA YA MRADI WA KUSAMBAZA MAJI KONGOWE HADI SOGA

UTANGULIZI

Mamlaka ya Majisafi na usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) imetekeleza mradi wa jumla ya Kilomita 5.05 kwa lengo la kuongeza msukumo wa maji kwenye bomba la inchi 6, linalopeleka maji kuhudumia wananchi wa kuanzia Kongowe hadi Soga eneo ambalo lilikuwa halitoi maji kama inavyostahili.

Mradi unategemea maji kutoka kwenye bomba kubwa la inchi 6 ambalo lililazwa kwa zaidi ya miaka mitano (5) kwa ajili ya kuhudumia baadhi ya wananchi wa Kongowe na maeneo yote ya Kigero, Vikuge, Msufini, Dengwa hadi Soga.

Ili kuondoa changamoto ya maji maeneo ya Kongowe hadi Soga, ulipendekezwa mradi huu wenye lengo la kuchepusha bomba eneo lililovamiwa na mkondo wa maji, kuweka mtandao wa mabomba eneo jipya bomba lilikochepushiwa, na kuongeza ukubwa wa kipenyo cha bomba na kuwa inchi 8 kutoka kwenye maunganisho kwa umbali wa Kilomita tatu (3) na kuungwa kwenye bomba lililopo la inchi 6.

UWEZO WA MRADI

Mradi huu wa maji wa Kongowe hadi Soga unasafirisha lita za ujazo milioni moja na laki mbili yanayotosheleza kuhudumia jumla ya Wananchi 7632, ambapo 1032 ni baadhi ya wananchi wa Kata ya Kongowe na 6,000 wa Kata ya Soga.

 

GHARAMA YA MRADI

Mradi huu umetekelezwa kwa kutumia fedha za ndani ya DAWASA, ambapo gharama zote kwa ununuzi wa vifaa pamoja na ujenzi wa bomba lenyewe kwa kutumia wataalamu wa ndani ni Sh milioni 339 bila VAT. (fedha kutoka wizarani).

 

UTEKELEZAJI WA MRADI

Mradi ulianza kutekelezwa Novemba 2020 na ulikamilika Februari 2021. Katika utekelezaji, shughuli zifuatazo zilifanyika:

  1. Ujenzi wa bomba la plastic inchi 8 pamoja na miundombinu kwa umbali wa Kilomita 3. Ujenzi wa bomba la plastic la inchi 3 pamoja na miundombinu kwa umbali wa Kilomita 0.85.
  2. Ujenzi wa bomba la plastic la inchi 2 pamoja na miundombinu yake umbali wa Kilomita 1.2.

Mradi umetekelezwa kwa jumla ya umbali wa Kilomita 5.05.

Mradi huu wa kupeleka maji Kongowe hadi Soga ni utekelezaji wa agizo la aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dr. John Magufuli.