Wizara ya Maji

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA)

TIRA Logo
MRADI WA MAJI DAR ES SALAAM YA KUSINI (BANGULO)
MRADI WA MAJI DAR ES SALAAM YA KUSINI (BANGULO)

TAARIFA YA MRADI WA MAJI DAR ES SALAAM YA KUSINI (BANGULO)

 

UTANGULIZI;

Mradi wa maji Dar es Salaam ya Kusini (Bangulo) ni mojawapo ya mradi wa kimkakati uliobuniwa na kusanifiwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) kwa lengo la kuongeza upatikanaji wa huduma ya majisafi kwa wananchi wa majimbo matano ya uchaguzi ambayo ni Ilala, Ubungo, Segerea, Kibamba na Temeke.

UTEKELEZAJI WA MRADI

Mradi ulisainiwa mnamo tarehe 17 mwezi Novemba mwaka 2023 kati ya DAWASA na Mkandarasi aliyeshinda zabuni, Kampuni ya M/S SINOHYDRO kutoka China na Mhandisi Mshauri M/S SCET TUNISIE akishirikiana na SMARCON ya Tanzania. Utekelezaji wa mradi umegawanyika katika awamu mbili.

Awamu ya kwanza ya utekelezaji mradi ilihusisha kazi zifuatazo;

  • Ujenzi wa kituo cha kusukuma maji kwenda kwenye tenki kitakachojengwa eneo la Kibamba.
  • Ulazaji wa bomba la inchi 28 kwa umbali wa kilomita 10.8 kutoka kwenye kituo cha kusukuma maji Kibamba mpaka Bangulo kwenye tenki.
  • Ujenzi wa tenki la kuhifadhi maji la lita milioni 9 litakalojengwa eneo la Bangulo.
  • Awamu ya kwanza ya mradi itazalisha lita milioni 23.33 za maji kwa siku.

Awamu ya pili ya utekelezaji wa mradi ilihusisha kazi zifuatazo:

  • Ujenzi wa matoleo 18 ya kutoa maji kutoka kwenye bomba kuu la kusafirisha na kusambaza maji.
  • Ujenzi wa tenki la lita milioni moja katika eneo la Mwanagati.
  • Uchimbaji na ulazaji wa bomba za ukubwa wa inchi 10 kutoka kwenye tenki kwa umbali wa kilomita 2.9 sambamba na ulazaji wa bomba mbalimbali za usambazaji maji katika maeneo ya Mwanagati.
  • Kazi ya kulaza bomba za usambazaji maji za ukubwa tofauti kuanzia inchi 16 hadi inchi 2 kwa umbali wa kilomita 281, kwa lengo la kufikisha huduma ya maji kwenye Kata za Kwembe, Charambe, Majohe, Chanika, Zingiziwa, Kivule, Kinyerezi na maeneo ya Buza, Msigani na Mbezi.
  • Awamu ya pili ya mradi inazalisha lita milioni 70.033 za maji kwa siku.