Wizara ya Maji

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA)

TIRA Logo
MRADI WA MAJI JET – BUZA
MRADI WA MAJI JET – BUZA

TAARIFA YA MRADI WA MAJI JET – BUZA

UTANGULIZI

Mradi wa maji Jet – Buza ni mojawapo ya mradi wa kimkakati uliotekelezwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) kwa lengo la kutoa huduma ya majisafi kwa wakazi wa Kata ya Kiwalani, Buza, Kilakala, Makangarawe, Yombo na Vituka zilizopo katika Wilaya ya Temeke.

Mradi wa maji Jet – Buza ulianza kutekelezwa kwa awamu mbalimbali ikiwemo awamu ya kwanza, ya pili na ya tatu ambapo awamu ya kwanza ilianza mwaka 2021.

Katika awamu ya kwanza ya mradi, usanifu wa mradi ulilenga kuhudumia Kata kuu tano ambazo ni Kiwalani, Kilakala, Yombo Vituka, Kigilagila na Buza.

 

UTEKELEZAJI WA MRADI

Awamu ya kwanza ya mradi imehusisha utekelezaji wa kazi mbalimbali zikiwemo;

•        Ujenzi wa bomba kubwa la kusafirisha maji kwa umbali wa kilomita 7.5.

•        Ujenzi wa mtandao wa mabomba ya kusambaza maji kwa wateja kwa umbali wa kilomita 42.

Awamu ya pili ya mradi imehusisha utekelezaji wa kazi mbalimbali zikiwemo;

•        Ulazaji wa mabomba ya kusambaza maji ya ukubwa wa inchi 8, 6, 4 na 2 kwa umbali wa kilomita 262 kwa wateja wa maeneo tajwa.

•        Uwekaji wa mfumo wa kutoa hewa kwenye bomba kubwa la kusafirisha maji.

 

1.2 WANUFAIKA WA MRADI

Utekelezaji wa mradi unalenga kunufaisha wakazi 175,000 wa Kata ya Kiwalani, Kilakala, Makangarawe, Yombo, Vituka, Buza na Kigilagila kwenye Wilaya ya Temeke.

Katika Kata ya Yombo vituka, mradi unahudumia wakazi wa mtaa wa Vituka, Magogoni, Sigara na Mzambarauni na kwa Kata ya Buza, mradi unahudumia mtaa wa Amani na mtaa wa Lulenge.

Awamu ya kwanza ya mradi imekamilika kwa asilimia 100. Kazi ya utekelezaji wa mradi kwa awamu ya pili na ya tatu inaendelea katika eneo la mradi.

1.3 GHARAMA ZA MRADI

Mradi wote wa Jet – Buza ambao umetekelezwa kwa awamu mbili, kwa gharama ya Tsh Bilioni 2.2.